Welcome

    HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

    .

    Social Icons

Loading...

TIMU YA UFARANSA KUFUNGUA PAZIA EURO CUP LEO...


Timu ya Ufaransa
PARIS, Ufaransa
TIMU ya taifa ya Ufaransa inafungua pazia la michuano ya Euro 2016 leo Ijumaa katika mtanange dhidi ya Romania huku ikiwa inapewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa wa mwaka huu. Mechi ya leo itaanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Timu nyingine zilizopo kwenye kundi moja na Ufaransa, ukiachana na Romania, ni Albania na Uswisi.
Kuelekea mchezo wa leo, Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, amesema: “Nawaamini wachezaji wangu. Mechi ya kwanza siyo ya kuamua lakini ni muhimu kwa sababu inatengeneza morali ya mechi zote.”
Timu yaRomania
Romania wanaonekana kuhangaika katika kufunga mabao lakini ukuta wao ni mgumu kupitika. Hatari kubwa ya Ufaransa ni katika ulinzi baada ya Raphael Varane na Lassana Diarra kuwa majeruhi. Laurent Koscielny na Adil Rami, wanaonekana ndiyo watakaochezeshwa leo katika ukuta wa kati lakini ni mara chache wamecheza pamoja na walipocheza walionyesha kutokujiamini na makosa kibao.

KAMA HUJAONA HII YA BIG KUTOANA JASHO NA NIVA HUKU KUPA AKISHUHUDIA... ACHIMENENGULE..



ACHIMENENGULE, Nimsemo uliozoeleka na kutambulika kupitia Bendi ya muziki wa dansi Tanzania ijulikanayo kama Tanzania one theatre au TOT. Ambao katika vibao vyao kulikuwa na kibwagizo kinachoitwa achimenengule kilichoanzishwa na Marehemu Banza Stone Mwana masanja.
Lakini jina hili limekuja kivingine, ACHIMENENGULE ni Filamu mpya Itakayouwa mitaani hivi karibuni kuptia kampuni ya SPLASH ambayo ni kambpuni pacha ya STEPS ENTERTAINMENT.
Filamu hii itawakutanisha wakali kama Zuberi Mohamed (NIVA)Idrisa Makupa ( KUPA)Luvole Matuvolwa (BIG), Hans wa Leo, ambaye ni msanii wa Bongo Flava na wengine wengi.
filamu hii itakuwa mtaani hivi karibu so usikose kupata nakalayako.
© Copyright SOKASPORT
Back To Top