Welcome

    HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

    .

    Social Icons

Loading...

KWASI, CHIRWA USO KWA USO ZANZIBAR...


KWA sasa wote wawili hawapo katika vikosi vya timu zao, lakini Januari mwakani straika Obrey Chirwa wa Yanga na beki Asante Kwasi wa Simba watakutana Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi.
Kaimu Kocha wa Simba, Masoud Djuma amepanga kumjumuisha Kwasi kwenye kikosi atakachokitumia katika Kombe la Mapinduzi mara baada ya mechi yao ya leo Jumamosi dhidi ya Ndanda FC.
Mechi za Kombe la Mapinduzi zinaanza leo kwa Mlandege kucheza na JKU huku Jamhuri ikicheza na Mwenge na Zimamoto dhidi ya Taifa Jang’ombe. Mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Kwasi ambaye ndiye aliyekuwa gumzo kwenye dirisha dogo, alisaini Msimbazi akitokea Lipuli FC iliyomuachia kwa dau la Sh25 milioni.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Djuma alisema; “Kwasi atajiunga na mazoezi ya pamoja na wenzake Jumatatu tukirejea kutoka Mtwara.”
Djuma alisema Kwasi ataanza mazoezi ya pamoja na wenzake akiwa tayari amemaliza programu ya mazoezi ya fitinesi ya gym na kukimbia ufukweni ambayo alimpatia.

Wakati huohuo, Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wake, Dismas Ten imesema straika wake Obrey Chirwa anawasili leo Jumamosi na keshokutwa Jumatatu ataungana na wenzake kwenda Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi.
“Chirwa atawasili kesho (leo) kutoka kwao Zambia, huyu hayupo katika kikosi kitakachocheza na Mbao (FC) Jumapili (kesho), lakini Jumatatu ataungana na wenzake kwenda Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi,” alisema Ten.

DROO KOMBE LA DUNIA NIGERIA KUANZA NA ARGENTINA TENA...

Nigeria wamepangwa kwenye kundi moja na Argentina kwa mara nyingine, Misri nao wakapangwa na Urusi na Uruguay baada ya droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanywa nchini Urusi.
Panama, ambao wanacheza Kombe la Dunia mara ya kwanza wamepangwa na Ubelgiji na England na Tunisia.
Iceland, walioshangaza wengi kwa kufuzu, wamepangwa kucheza na Nigeria, Croatia na Argentina katika Kundi D.
Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Urusi na Saudi Arabia.

Droo kamili ya Kombe la Dunia:

  • Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay
  • Kundi B: Ureno, Uhispania, Morocco, Iran
  • Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark
  • Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
  • Kundi E: Brazil, Uswizi, Costa Rica, Serbia
  • Kundi F: Ujerumani , Mexico, Sweden, Korea Kusini
  • Kundi G: Ubelgiji , Panama, Tunisia, England
  • Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan.

Nani wanadhaniwa kushinda?
Mabingwa watetezu Ujerumani wanapigiwa upatu kushinda, wakifuatwa na Brazil, Uhispania, Argentina, Ufaransa, Ubelgiji na kisha England.
Ujerumani chini ya Joachim Low wanatafuta kuwa nchi ya kwanza kushinda Kombe la Dunia mtawalia tangu Brazil wakiwa na Pele 1958 na 1962.
Nani alivutia zaidi mechi za kufuzu?
Ujerumani hawajashindwa mechi hata moja ya fainali za au za kufuzu kwa Kombe la Dunia tangu nusu fainali ya 2010 dhidi ya Uhispania.
Walimaliza michuano ya kufuzu 2018 wakiwa wameshinda mechi 10 kati ya kumi walizocheza, na kufunga mabao 43. Walifungwa mara nne pekee.
Ubelgiji, Uhispania na England wote walimaliza mechi za kufuzu Ulaya bila kushindwa.
Brazil walitamba mechi za kufuzu Kombe la Dunia - lakini baada ya kumuondoa meneja Dunga na kumuingiza Tite.
Barani Asia, Iran walipitia makundi mawili bila kushindwa - mechi 18 bila kushindwa, ambapo mechi 12 kati ya hizo hawakufungwa bao hata moja.
Morocco walifuzu bila kufungwa bao hata moja katika kundi lao la kufuzu Afrika, ambapo walimaliza juu ya Ivory Coast.
Nani wanacheza mara ya kwanza?
Iceland ndiyo nchi ya kwanza pekee yenye raia ambao ni chini ya milioni moja kuwahi kufika Kombe la Dunia.
Hawakuwa wamefuzu kwa michuano mikubwa kabla ya kushiriki Euro 2016 ambapo waliwalaza England katika safari yao ya kufika robo fainali.
Panama, taifa la Amerika ya Kati, nao walifika Kombe la Dunia baada ya bao la ushindi la dakika ya 88 dhidi ya Costa Rica, bao ambalo pia liliwazuia Marekani kufuzu.
Nani miamba ambao wameachwa nje?
Walioshangaza zaidi walitoka Ulaya.
Mabingwa mara nne Italia walishindwa kufuzu kwa mara ya kwanza tangu 1958 baada ya kuondolewa na Sweden.
Uholanzi pia walishindwa kufuzu.
Jamhuri ya Czech, Wales, Scotland, Austria, Bosnia-Herzegovina na Uturuki ni miongoni mwa nchi nyingine za Ulaya zilizoshindwa kufuzu hatua ya makundi.
Jamhuri ya Ireland, Ireland Kaskazini na Ugiriki pia waliondolewa kwenye mechi za muondoano za kufuzu baada ya makundi.
Jimbo la Concacaf, Marekani walishindwa kufuzu kwa mara ya kwanza tangu 1986.
Barani Afrika, Ivory Coast, Cameroon na Ghana - wote ambao walishiriki Kombe la Dunia Brazil 2014 - pia hawakufuzu.
Chile, walioorodheshwa nafasi ya tisa duniani, pia walishindwa kufuzu.
Tiketi zinauzwaje?
Fifa wamepokea maombi 3.5 milioni ya tiketi, 300,000 yakiwa maombi ya tiketi za mechi ya fainali uwanjani Luzhniki.
Asilimia 57 ya maombi yametoka kwa wakazi wa je ya Urusi.
Tiketi ya bei nafuu zaidi ya fainali Kombe la Dunia ambayo raia asiye wa Urusi anaweza kununua ni ya £345.

HIZI HAPA PICHA MAITI YA NDIKUMANA


ALIYEKUWA mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana (katauti) (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo.

Habari zinasema kuwa Ndikumana ambaye pia alikuwa Kocha msaidizi wa timu ya Lion Sport ya nchini Rwanda, jana tu alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida, lakini inasemekana kuwa alikuwa analalamika maumivu ya moyo na akaomba kinywaji baridi lakini ghafla akawa anaishiwa nguvu na akaanguka na kufariki dunia.


Mpaka anakutwa na umauti alikuwa akicheza katika timu ya APOP Kinyras Peyias FC ya  Cyprus.  Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na Uwoya kwa mengi na alikuwa ndiye mkewe aliyefunga naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja  wa kiume anayeitwa Krish.

KENYA YANYANG'ANYWA FURSA KUANDAA MECHI ZA CHAN 2018

Kenya imepokonywa fursa ya kuandaa mashindano ya ubingwa wa Afrika wa mwaka 2018 (CHAN) kufuatia mkutanoa wa kamati kuu ya Caf uliofanyika Accra.
Hatua hiyo ilitangazwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mkutano wa siku moja uliioongozwa na rais wa Caf Ahmad.
Caf inasema uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuchelewa kwa ripoti za ukaguzi kadha uliofanywa nchini Kenya.
Kinyanganyiro hicho ambacho kitashirikisha timu 16 kinatarajiwa kuanza tarehe 12 Januari hadi Februari mwaka 2018.
Timu ya ukaguzi ya Caf ilizuru Kenya kuanzia tarehe 11 hadi 17 mwezi huu, na kupata kuwa ni uwanja mmoja tu kati ya viwanja vinne uliokuwa tayari kwa michuano hiyo.
Shirikisho la kandanda nchini Kenya (FKF) linasisitiza kuwa lilifanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa mashindano ya CHAN mwaka 2018 yangewezekana kwa Kenya na eneo lote la Afrika Mashariki.

TIKETI ZA KWANZA ZAANZA KUUZWA - KOMBE LA DUNIA 2018 - RUSSIA

Kundi la kwanza la tiketi za fainali za Kombe la Dunia 2018 ambazo zitachezewa nchini Urusi zilianza kuuzwa Alhamisi.
Mashabiki wa soka wanaweza kuwasilisha maombi ya kununua tiketi hizo kupitia tovuti ya Fifa.
Tiketi hizo zitauzwa kwa awamu mbili.
Bei ya tiketi hizo itakuwa ni kuanzia £79 kwa mechi za raundi ya pili hatua ya makundi hadi £829 kwa fainali yenyewe ambayo itachezewa Moscow.
Kwa kufuata sera za awali za uuzaji wa tiketi, wakazi wa urusi watakuwa na aina maalum za tiketi ambazo bei yake itaanzia £17.
Tiketi ghali zaidi zitakuwa za mechi ya fainali yenyewe ambazo zitauzwa £829.
Hilo litakuwa ni ongezeko la £151 ukilinganisha na tiketi za mechi sawa za fainali ya mwaka 2014 ambayo ilichezewa Rio de Janeiro nchini Brazil.
"Tumeweka mfumo wa kutoa tiketi ambao utawapa mashabiki nafasi sawa ya kujipatia tiketi," katibu mkuu wa Fifa Fatma Samoura amesema.

MECHI YA ARSENAL NA COLOGNE ILIVYOVAMIWA...

Mechi ya Arsenal dhidi ya Cologne katiika kombe la Yuropa ilikumbwa na ghasia na kusababisha kucheleweshwa kwa saa moja.
Maelfu ya mashabiki wa kigeni waliwasili katika uwanja huo bila tiketi na kulikuwa na ghasia kati ya mashabiki na wapokezi wao ndani ya uwanja huo baada ya mlango kufunguliwa.
Maafisa wa polisi walisema kuwa watu watano walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika ghasia.
Kulikuwa hakuna ripoti zozote za ghasia wakati wa mechi hiyo ambayo Arsenal ilishinda magoli 3-1.
Timu hiyo ya Ujerumani ilikuwa imepewa tiketi 2,900 pekee.
Lakini takriban mashabiki 20,000 wa timu hiyo waliingia na kusimamisha biashara mjini London nyakati za mchana Alhamisi.
Hatahivyo hivyo mechi hiyo ilianza baada ya kucheleweshwa kwa saa moja.

MAN CITY WALIVYOIFUMUA LIVEPOOL...

Manchester City ime uraruwa ulinzi hafifu wa Liverpool na kunyakua ushindi mkubwa dhidi ya wageni wake wa kikosi cha wachezaji 10 Liverpool, na kufanikiwa kukwea kwenye orodha ya ligi.
Sergio Aguero alifungua mvua ya mikwaju kwa kumchenga kipa wa Liverpool Simon Mignolet.
Sadio Mane alitolewa uwanjani baada ya kunyanyua mguu wake uliomgonga kipa wa City, Ederson, aliyetibiwa uwanjani kwa dakika 10.
Gabriel Jesus aliongeza jingine na Leroy Sane kumalizia kwa mawili ya mwisho na kukamilisha ushindi wa 5-0.
Kevin de Bruyne alitoa pasi safi kwa goli la ufunguzi la Aguero na pia alimtambua na kumpa pasi Jesus aliyekuwa wazi na kufanikiwa kuifungia City katika muda wa ziada baada ya kujeruhiwa kwa Ederson.
Ushindi huu unakiinusha kikosi cha Pep Guardiola juu ya mahasimu Manchester United kwenye ligi, wanaokuwa wageni wa Stoke baadaye Jumamosi.
Na unahakikisha kushindwa kwa mara ya kwanza katika msimu kwa kikosi cha Jurgen Klopp.
© Copyright SOKASPORT
Back To Top