Welcome

    HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

    .

    Social Icons

Loading...

THAMANI YA MBWANA SAMATTA YAZIDI KUPANDA ULAYA

NEEMA imezidi kumuangukia mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, baada ya thamani yake kuongezeka kwa mara nyingine.
Samatta aliyewahi kuichezea Simba kabla ya kutimkia TP Mazembe, thamani yake ilianza kupanda Machi 22, mwaka huu na kufikia euro milioni 2.2 (zaidi ya Sh bilioni 5). Mtanzania huyo, alijiunga na Genk Januari 29, mwaka jana kwa ajili ya kuichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Ubelgiji.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Transfermarket thamani ya mshambuliaji huyo ilipanda juzi Jumatatu na kufikia euro milioni 3 (sawa na shilingi bilioni 7.1)
Ni historia kubwa kwa mshambuliaji huyo Mtanzania kuingia kwenye ushindani wa wacheza soka duniani ambao thamani yao inaongezeka kwenye mauzo.
Samatta, thamani yake imeongezeka baada ya kuifungia mabao sita timu yake ya Genk kwenye michezo saba aliyocheza hivi karibuni ukiwemo mmoja ule wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wakati Taifa Stars iliposhinda mabao 2-0 huku mabao yote yakifungwa na mshambuliaji huyo wa Genk.
Mabadiliko hayo ya thamani yamefanyika Machi 30, mwaka huu katika wiki aliyofanya vizuri kwa kufunga mabao matatu.
Alifunga mabao mawili dhidi ya Botswana siku ya Jumamosi ya Machi 25 kabla ya kuwahi Ubelgiji na kufunga bao wikiendi iliyopita katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata.
HII HAPA DAMU TULIZA MOYO YA MUSSA SIKABWE

LIVERPOOL KUMSAFIRISHA SADIO MANE KWA NDEGE BINAFSI

Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya kibinafsi mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kushiriki mechi na viongozi wa Ligi Chelsea.
Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakati wa mechi ya robo fainali siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.
Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushiriki mechi za kimataifa.
Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.
© Copyright SOKASPORT
Back To Top