Welcome

    HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

    .

    Social Icons

Loading...

HII HAPA YA MKUFUNZI WA BARCELONA KUJIUZULU...

Mkufunzi wa klabu ya Barcelona Luis Enrique ametangaza kwamba atabwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu.
Enrique atakuwa amehudumu kama meneja wa klabu hiyo kwa misimu mitatu .
Aliishindia klabu hiyo kombe la vilabu bingwa na mataji mengine mawili alipojiunga na Barcelona na kuwasaidia kushinda makombe 2 mwaka uliopita.
Lakini licha ya klabu hiyo kuongoa katika jedwali la ligi Barcelona iko katika hatari ya kubanduliwa katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu huu baada ya kufungwa 4-0 na Prais St-Germain.
Enrique amesema kuwa sababu kuu ya yeye kutaka kujiuzulu ni kwamba anahitaji kupumzika.

ROGOBERT SONG SHUJAA WA CAMEROON MWENYE REKODI ZAKUMWAGA AFCON

HUWEZI ukazizungumzia rekodi za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) bila kulitaja jina la Mcameroon, Rigobert Song (pichani). Jamaa ana rekodi kibao kwenye michuano hiyo pamoja na nchini kwao Cameroon kwa ujumla.
Rigobert Song Bahanag, aliye­zaliwa Julai Mosi, 1976, alikuwa mchezaji wa Cameroon kwa miaka 17 kuanzia 1993 hadi 2010.
Akijulikana duniani kote kutokana na uwezo wake wa kukaba, Song, 40, mara nyingi alicheza kama beki wa kati lakini aliweza pia kucheza kama beki wa kulia kwa ustadi mkubwa.
Rekodi ya kwan­za aliyonayo Afcon ni kwamba, alicheza kwenye michuano nane ya Afcon huku akiwa na­hodha katika michuano mitano (michuano am­bayo hakuwa nahodha ni ya Afrika Kusini 1996, Burkina Faso 1998 na 2010). Hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivyo.
Song pia anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi mfu­lulizo katika Afcon. Alicheza mechi 35 mfululizo katika kikosi cha kwanza cha Cameroon. Pamoja na hayo, alitwaa ubingwa wa Afcon mara mbili; 2000 na 2002.
Mwaka 2009, Song alistaafishwa unahodha na kocha mpya Paul Le Guen, ambaye alimpa kitambaa hi­cho Samuel Eto’o, baadaye kocha huyo akaishangaza Cameroon kwa kumuweka benchi Song ambaye kabla, hakuwahi kuwekwa benchi kwa miaka 11 akiitumikia Cam­eroon.
Akiwa ameichezea C am­eroon mechi 137, Song pia anashikilia re­kodi ya mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya Cameroon na amecheza katika michuano minne ya Kombe la Dunia; 1994, 1998, 2002 na 2010.
Song alianza maisha yake ya soka akiwa Metz na aliisaidia timu hiyo ya Ufaransa kutwaa taji la Kombe la Ligi (Coupe de la Ligue) mwaka 1996. Baada ya kutokeza kwenye Kombe la Dunia 1998, Song alijiunga na Salernitana, am­bayo ilikuwa imepanda kucheza Ligi Kuu ya Italia (Serie A).
Akiwa pamoja na Zinedine Zi­dane, Song ni mchezaji pekee ku­tolewa nje kwa kadi nyekundu kati­ka michuano miwili ya Kombe la Dunia, mara ya kwanza dhidi ya Brazil mwaka 1994 na mara ya pili dhidi ya Chile mwaka 1998. Pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kutolewa kwa kadi uwanjani kwenye Kombe la Dunia, alikuwa na miaka 17.
Song ambaye mashabiki Watu­ruki walimuita jina la utani la ‘Big Chief’, ni mjomba wa kiungo mkabaji Mcameroon anayeichezea Rubin Kazan ya Urusi, Alex Song.
Akiwa ni Mcameroon wa kwanza kuichezea Liverpool, Song alikuba­lika vilivyo kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao walikubali nguvu zake, staili na juhudi zake na mara kad­haa walikuwa wakimwimbia: “Tuna Song mmoja tu.” Msimu wa 1999- 2000 alikosekana kwa miezi mitatu kutokana na majukumu ya timu ya taifa ambapo alikwenda kuiongoza Cameroon kutwaa ubingwa wa Af­con 2000 akiwa nahodha huku aki­funga penalti ya kuamua mshindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Nigeria.
Song alishuhudia mengi, moja­wapo ni kuwa katika michuano ya Kombe la Mabara 2003, mchezaji mwenzake Marc-Vivien Foé alian­guka uwanjani akimshuhudia na baadaye aka­fariki dunia na kuzua si­manzi kubwa duniani.
Katika Af­con 2008, Song aliiongo­za Cameroon hadi fainali lakini alifanya kosa kubwa lililozaa bao pekee la Misri lililofungwa na Mohamed Aboutrika na kuiko­sesha timu yake kombe. Wakati Wamisri wakishangilia, Song aliu­funika uso wake kwa jezi akilia kwa uchungu.
Baada ya hapo, Song aliendelea kufanya makosa mengi ya ajabu. Katika Afcon 2010, alifanya kosa lililosababisha Gabon wakapata bao na kushinda 1-0 lakini katika mchezo mwingine dhidi ya Zambia aliunganisha krosi kwenye goli lake mwenyewe. Timu ilifika robo fain­ali lakini ikatolewa kwenye dakika 30 za nyongeza na Misri.
Song alistaafu kuichezea Cam­eroon mwaka 2010 akiwa ameche­za mechi 137 na kufunga mabao matano. Kwa ngazi ya klabu pia alistaafu mwaka 2010.
 MATAJI
FC Metz: Coupe de la Ligue: 1995-96. Galatasaray: Süper Lig: 2005-06, 2007-08, Turkish Cup: 2005. Trabzonspor: Turkish Cup: 2009, Turkish Cup: 2010. Cam­eroon: Afcon (2): 2000, 2002.
MAISHA BINAFSI
Baba yake Song, Paul Song, alifa­riki dunia wakati Song akiwa mtoto. Hamjui baba yake, lakini alikuwa akiyatoa mabao yake kwake. Song amemuoa mrembo Esther Song na wana watoto wanne. Hivi sasa wanaishi Liverpool. Song alipata shambulio la moyo Oktoba 3, 2016 na alilazwa Cameroon. Alipoteza fahamu kwa siku mbili lakini mwis­honi mwa mwaka iliripotiwa hali yake imeimarika.
ANACHOKIFANYA KWA SASA
Hivi sasa Song ni kocha wa timu ya taifa ya Cameroon ‘A’ ambayo ni ya wachezaji wa­naocheza ndani ya Cameroon.

BEKI WA SIMBA AANGUKA BAFUNI NA KUPASUKA VIBAYA

Mchezaji wa Coastal Union,Hamad Juma akiwa ameanguka chini huku mchezaji wa Simba, Hassan Kessy (kulia) akichanja mbuga kuelekea golini kwao mechi ya Ligi Kuu msimu uliopita.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
BEKI mpya wa kulia wa Simba, Hamad Juma, jana asubuhi alianguka bafuni akiwa nyumbani kwake na kusababisha achanike kisogoni kwake.
Juma alijiunga na Simba msimu huu wa Ligi Kuu Bara akisaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Coastal Union baada ya mkataba wake kumalizika.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo kinasema jana jioni na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, tukio hilo lilitokea nyumbani kwake kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam alipokwenda kulazwa.
Manara alisema, beki huyo mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo, madaktari walishauri alazwe kutokana na damu nyingi zilizokuwa zinamtoka.
“Hamad ameanguka na amepoteza damu nyingi sana, alipata matatizo hayo akiwa nyumbani kwake wakati anaingia bafuni na hivi sasa ninavyoongea na wewe yupo Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu.
“Madaktari wamelazimika kumuongezea damu beki huyo kutokana na kutoka nyingi, lakini tunashukuru hivi sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya haraka na madaktari hao, amelazwa wodi namba tano,” alisema Manara.
Aidha alipotafutwa Daktari Mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe kuzungumzia hilo, alisema: “Ninaomba nipigie baadaye hivi sasa nipo hospitali na nipo ‘busy’ na mgonjwa, ninaomba umpigie Manara atakupa taarifa nzima.”
© Copyright SOKASPORT
Back To Top